2 Petro 1:1-2
2 Petro 1:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi Simoni Petro, mtumishi na mtume wa Yesu Kristo, nawaandikia nyinyi ambao, kwa wema wake Mungu wetu na Mwokozi Yesu Kristo, mmejaliwa imani ileile ya thamani kuu tuliyojaliwa sisi. Nawatakieni neema na amani tele katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.
2 Petro 1:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waliopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.
2 Petro 1:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waliopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.
2 Petro 1:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Simoni Petro, mtumishi na mtume wa Yesu Kristo: Kwa wale ambao kwa njia ya haki ya Mungu na Mwokozi wetu Yesu Kristo mmepokea imani iliyo na thamani kama yetu: Neema na amani iwe kwenu kwa wingi katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.