1 Timotheo 6:20-21
1 Timotheo 6:20-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Timotheo, tunza salama yote yale uliyokabidhiwa. Jiepushe na majadiliano ya kidunia na ubishi wa kipumbavu juu ya kile wanachokiita watu wengine “Elimu.” Maana wengine wamejidai kuwa na hiyo elimu, na matokeo yake wamepoteza imani. Nawatakieni nyote neema!
1 Timotheo 6:20-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na mazungumzo yasiyo ya kimungu, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo; ambayo wengine kwa kuikiri wamepoteza Imani. Neema na iwe pamoja nanyi.
1 Timotheo 6:20-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo; ambayo wengine wakiikiri hiyo wameikosa Imani. Neema na iwe pamoja nanyi.