1 Wathesalonike 2:3-4
1 Wathesalonike 2:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Jambo tunalosisitiza kwenu si jambo linalotegemea uongo au nia mbaya; wala hatupendi kumdanganya mtu yeyote. Sisi twanena daima kama atakavyo Mungu kwani yeye alituona kwamba tunafaa, akatukabidhi hii Habari Njema. Si nia yetu kuwapendeza watu hata kidogo, bali twataka kumpendeza Mungu ambaye anajua mioyo yetu mpaka ndani.
1 Wathesalonike 2:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala ya uchafu, wala ya hila; bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu.
1 Wathesalonike 2:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala ya uchafu, wala ya hila; bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu.
1 Wathesalonike 2:3-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa maana himizo letu halikutokana na hila wala nia mbaya au udanganyifu. Kinyume chake, tulinena kama watu tuliokubaliwa na Mungu tukakabidhiwa Injili. Sisi hatujaribu kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu, yeye ayachunguzaye mawazo ya ndani sana ya mioyo yetu.