1 Samueli 15:9
1 Samueli 15:9 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini Shauli na watu wake hawakumuua Agagi, wala kondoo bora kabisa, ng'ombe wazuri, ndama, wanakondoo na chochote kile kilichokuwa kizuri hawakukiangamiza. Lakini vitu vyote vibaya na visivyo na thamani waliviangamiza.
1 Samueli 15:9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na chochote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali chochote kilichokuwa kibaya na kisichofaa, ndicho walichoangamiza kabisa.
1 Samueli 15:9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng’ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa.
1 Samueli 15:9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini Sauli na hilo jeshi wakamhifadhi hai Agagi na kondoo na ngʼombe walio wazuri, mafahali na wana-kondoo walionona kila kitu kilichokuwa kizuri. Hivi vitu hawakuwa radhi kuviangamiza kabisa, bali kila kitu kilichodharauliwa na kilicho dhaifu wakakiangamiza kabisa.