1 Samueli 15:30-31
1 Samueli 15:30-31 Biblia Habari Njema (BHN)
Shauli akajibu, “Nimefanya dhambi. Hata hivyo, unistahi sasa mbele ya wazee wa watu wangu na Waisraeli. Niruhusu nirudi pamoja nawe ili nikamwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.” Basi, Samueli akarudi pamoja naye mpaka Gilgali na Shauli akamwabudu Mwenyezi-Mungu.
1 Samueli 15:30-31 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa, nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu BWANA, Mungu wako. Basi Samweli akarudi na kuandamana na Sauli; naye Sauli akamwabudu BWANA.
1 Samueli 15:30-31 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa, nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu BWANA, Mungu wako. Basi Samweli akarudi na kuandamana na Sauli; naye Sauli akamwabudu BWANA.
1 Samueli 15:30-31 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sauli akajibu, “Nimetenda dhambi. Lakini tafadhali niheshimu mbele ya wazee wa watu wangu na mbele ya Israeli; rudi pamoja nami, ili nipate kumwabudu BWANA Mungu wako.” Hivyo Samweli akarudi pamoja na Sauli, naye Sauli akamwabudu BWANA.