1 Samueli 15:26-27
1 Samueli 15:26-27 Biblia Habari Njema (BHN)
Samueli akamjibu: “Kamwe, siwezi kurudi pamoja nawe. Wewe umeikataa amri ya Mwenyezi-Mungu, naye amekukataa kuwa mfalme juu ya Israeli.” Samueli alipogeuka ili aende zake, Shauli akashika pindo la vazi lake, nalo likapasuka.
1 Samueli 15:26-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli. Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka.
1 Samueli 15:26-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli. Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka.
1 Samueli 15:26-27 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini Samweli akamwambia, “Sitarudi pamoja nawe. Umelikataa neno la BWANA, naye BWANA amekukataa wewe, usiendelee kuwa mfalme juu ya Israeli!” Samweli alipogeuka ili aondoke, Sauli akangʼangʼania pindo la joho lake, nalo likararuka.