1 Samueli 15:24-25
1 Samueli 15:24-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Shauli akamwambia Samueli, “Nimetenda dhambi. Nimeasi amri ya Mwenyezi-Mungu na amri yako, kwa sababu niliwaogopa watu, nikawatii wao. Lakini sasa nakuomba, unisamehe dhambi yangu. Niruhusu nirudi pamoja nawe ili niweze kumwabudu Mwenyezi-Mungu.”
1 Samueli 15:24-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeivunja amri ya BWANA, pia na maneno yako; kwa sababu niliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao. Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu BWANA.
1 Samueli 15:24-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya BWANA, pia na maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao. Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu BWANA.
1 Samueli 15:24-25 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo Sauli akamwambia Samweli, “Nimetenda dhambi. Nimevunja amri ya BWANA na maagizo yako. Niliwaogopa watu na kwa hiyo nikafanya walivyotaka. Sasa ninakusihi usamehe dhambi yangu, nawe urudi pamoja nami, ili nipate kumwabudu BWANA.”