1 Samueli 15:20-21
1 Samueli 15:20-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Shauli akajibu, “Nimetii sauti ya Mwenyezi-Mungu. Nilikwenda kule alikonituma Mwenyezi-Mungu; nimemleta Agagi mfalme wa Waamaleki, na nimewaangamiza kabisa Waamaleki. Lakini watu walichukua nyara: Kondoo, ng'ombe na vitu vyote bora vilivyotolewa viangamizwe ili kumtambikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, huko Gilgali.”
1 Samueli 15:20-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya BWANA, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng'ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, huko Gilgali.
1 Samueli 15:20-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya BWANA, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng’ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, huko Gilgali.
1 Samueli 15:20-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sauli akasema, “Lakini nilimtii BWANA. Nilikamilisha ile kazi ambayo BWANA alinituma. Niliwaangamiza Waamaleki kabisa na kumleta Agagi mfalme wao. Askari walichukua kondoo na ngʼombe kutoka kwenye nyara, zile ambazo ni nzuri sana zimewekwa wakfu kwa Mungu, ili zitolewe dhabihu kwa BWANA Mungu wako huko Gilgali.”