1 Samueli 15:14-15
1 Samueli 15:14-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Samueli akamwambia, “Mbona nasikia mlio wa kondoo na ng'ombe?” Shauli akajibu, “Watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe bora kabisa ili kumtambikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, lakini wengine wote tumewaangamiza.”
1 Samueli 15:14-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Samweli akasema, Maana yake nini basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa.
1 Samueli 15:14-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Samweli akasema, Maana yake nini, basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng’ombe ninaousikia? Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng’ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa.
1 Samueli 15:14-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini Samweli akasema, “Nini basi huu mlio wa kondoo masikioni mwangu? Huu mlio wa ngʼombe ninaousikia ni kitu gani?” Sauli akajibu, “Askari wamewaleta kutoka kwa Waamaleki, waliwaacha wale kondoo na ngʼombe wazuri ili kuwatoa dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, lakini tuliwaangamiza kabisa wengine wote.”