1 Wafalme 3:2-3
1 Wafalme 3:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Kabla yake, watu walikuwa wakitoa tambiko vilimani, kwa kuwa nyumba ya Mungu ilikuwa bado haijajengwa. Solomoni alimpenda Mwenyezi-Mungu, akazingatia maongozi ya Daudi, baba yake; ila tu, naye ilimbidi kutoa tambiko na kufukiza ubani vilimani.
1 Wafalme 3:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ila watu walikuwa wakitoa dhabihu katika mahali pa juu, kwa sababu haikuwapo nyumba iliyojengwa kwa jina la BWANA, hata siku zile. Sulemani naye akampenda BWANA, akienda katika amri za Daudi babaye, ila hutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.
1 Wafalme 3:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ila watu walikuwa wakichinja dhabihu katika mahali pa juu, kwa sababu haikuwapo nyumba iliyojengwa kwa jina la BWANA, hata siku zile. Sulemani naye akampenda BWANA, akienda katika amri za Daudi babaye, ila hutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.
1 Wafalme 3:2-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hata hivyo, watu bado walikuwa wakitoa dhabihu huko kwenye vilima, kwa sababu Hekalu lilikuwa bado halijajengwa kwa ajili ya Jina la BWANA. Solomoni akaonyesha upendo wake kwa BWANA kwa kuenenda sawasawa na amri za Daudi baba yake, ila yeye alitoa dhabihu na kufukiza uvumba huko mahali pa juu.