1 Yohane 5:1-2
1 Yohane 5:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu. Kila anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu: Kwa kumpenda Mungu na kuzitii amri zake
1 Yohane 5:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. Katika hili tunajua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.
1 Yohane 5:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.