1 Wakorintho 12:29-31
1 Wakorintho 12:29-31 Biblia Habari Njema (BHN)
Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote ni wenye kipaji cha kufanya miujiza? Je, wote ni wenye kipaji cha kuponya? Je, wote ni wenye kipaji cha kusema lugha ngeni? Je, wote hufafanua lugha? Muwe basi, na tamaa ya kupata vipaji muhimu zaidi. Nami sasa nitawaonesheni njia bora zaidi kuliko hizi zote.
1 Wakorintho 12:29-31 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri? Jitahidini sana kupata karama zilizo kuu. Na nitawaonesheni njia iliyo bora zaidi.
1 Wakorintho 12:29-31 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri? Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora.
1 Wakorintho 12:29-31 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Je, wote ni mitume? Je, wote ni manabii? Je, wote ni walimu? Je, wote wanatenda miujiza? Je, wote wana karama ya kuponya? Je, wote hunena kwa lugha mpya? Je, wote wanatafsiri? Basi tamanini sana karama zilizo kuu. Nami nitawaonyesha njia iliyo bora zaidi.