1 Wakorintho 12:16-17
1 Wakorintho 12:16-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Kama sikio lingejisemea: “Kwa vile mimi si jicho, basi mimi si mali ya mwili,” je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La! Kama mwili wote ungekuwa jicho, sikio lingekuwa wapi? Na kama mwili wote ungekuwa sikio, mtu angewezaje kunusa?
1 Wakorintho 12:16-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si wa mwili; je! Linakuwa si la mwili kwa sababu hiyo? Kama mwili wote ukiwa jicho, kuko wapi kusikia? Kama wote ni sikio kuko wapi kunusa?
1 Wakorintho 12:16-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo? Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa?
1 Wakorintho 12:16-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Na kama sikio lingesema, “Kwa kuwa mimi si jicho, basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya hilo sikio lisiwe sehemu ya mwili. Kama mwili wote ungelikuwa jicho, kusikia kungekuwa wapi? Au kama mwili wote ungelikuwa sikio, kunusa kungekuwa wapi?