1 Mambo ya Nyakati 17:7-8
1 Mambo ya Nyakati 17:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa hiyo basi, mwambie mtumishi wangu Daudi: ‘Mwenyezi-Mungu wa majeshi anasema hivi: Nilikutoa malishoni ulipokuwa unawachunga kondoo, ili uwe mkuu wa watu wangu Israeli. Tangu wakati huo nimekuwa pamoja nawe kokote ulikokwenda na nimewaangamiza maadui zako wote mbele yako. Nitakufanya kuwa maarufu kama wakuu wengine wa dunia.
1 Mambo ya Nyakati 17:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi sasa ndivyo utakavyomwambia mtumishi wangu Daudi, BWANA wa majeshi asema hivi, Nilikutwaa kutoka machungani, hata katika kuwafuata kondoo ili uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli; nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina, kama jina la hao wakuu walioko duniani.
1 Mambo ya Nyakati 17:7-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi sasa ndivyo utakavyomwambia mtumishi wangu Daudi, BWANA wa majeshi asema hivi, Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo ili uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli; nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina, kama jina la hao wakuu walioko duniani.
1 Mambo ya Nyakati 17:7-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: Nilikuchukua machungani na kutoka kuandama kondoo ili uwatawale watu wangu Israeli. Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani.