1 Mambo ya Nyakati 17:25-26
1 Mambo ya Nyakati 17:25-26 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana ee Mungu wangu nimepata ujasiri kukuomba kwa sababu wewe, umenifunulia ukisema ya kwamba utanijengea nyumba. Sasa ee Mwenyezi-Mungu, wewe ndiwe Mungu, umeniahidi mimi mtumishi wako jambo hili jema
1 Mambo ya Nyakati 17:25-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa kuwa wewe, Ee Mungu wangu, umenifunulia mimi mtumishi wako ya kuwa utanijengea nyumba; kwa hiyo mimi mtumishi wako nimeona vema moyoni mwangu kuomba mbele yako. Na sasa, Ee BWANA, wewe ndiwe Mungu, nawe umemwahidia mtumishi wako jambo hili jema
1 Mambo ya Nyakati 17:25-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa kuwa wewe, Ee Mungu wangu, umenifunulia mimi mtumwa wako ya kuwa utanijengea nyumba; kwa hiyo mimi mtumwa wako nimeona vema moyoni mwangu kuomba mbele yako. Na sasa, Ee BWANA, wewe ndiwe Mungu, nawe umemwahidia mtumwa wako jambo hili jema
1 Mambo ya Nyakati 17:25-26 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Wewe, Mungu wangu, umemfunulia mtumishi wako Daudi kwamba utamjengea yeye nyumba. Hivyo mtumishi wako amekuwa na ujasiri wa kukuomba maombi haya. Ee BWANA, wewe ndiwe Mungu! Umemwahidi mtumishi wako mambo haya mazuri.