1 Mambo ya Nyakati 17:23-24
1 Mambo ya Nyakati 17:23-24 Biblia Habari Njema (BHN)
“Basi sasa, ewe Mwenyezi-Mungu, liimarishe milele neno lako ulilosema kunihusu mimi mtumishi wako na kuhusu jamaa yangu. Nalo jina lako litatukuzwa milele, nao watu watasema, ‘Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, ndiye Mungu wa Israeli!’ Na jamaa yangu, mimi Daudi mtumishi wako, itaimarika mbele yako.
1 Mambo ya Nyakati 17:23-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi sasa, Ee BWANA, neno lile ulilolinena kuhusu mtumishi wako, na kuhusu nyumba yake, na lifanywe imara milele, ukafanye kama ulivyosema. Jina lako na liwe imara, likatukuzwe milele, kusema, BWANA wa majeshi ndiye Mungu wa Israeli, naam, Mungu juu ya Israeli; na hiyo nyumba ya Daudi mtumwa wako imefanywa imara mbele zako.
1 Mambo ya Nyakati 17:23-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi sasa, Ee BWANA, neno lile ulilolinena katika habari za mtumwa wako, na katika habari za nyumba yake, na lifanywe imara milele, ukafanye kama ulivyosema. Jina lako na liwe imara, likatukuzwe milele, kusema, BWANA wa majeshi ndiye Mungu wa Israeli, naam, Mungu juu ya Israeli; na hiyo nyumba ya Daudi mtumwa wako imefanywa imara mbele zako.
1 Mambo ya Nyakati 17:23-24 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Sasa basi, BWANA ahadi uliyoweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake na uithibitishe milele. Fanya kama ulivyoahidi, ili ithibitike na jina lako litakuwa kuu milele. Kisha watu watasema, ‘BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu aliye juu ya Israeli, ndiye Mungu wa Israeli.’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itafanywa imara mbele zako.