1 Mambo ya Nyakati 17:19-20
1 Mambo ya Nyakati 17:19-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, kwa ajili ya mtumishi wako na kwa kufuatana na moyo wako mwenyewe, umeyatenda hayo makuu yote, ili yajulikane hayo matendo makuu yote. Hakuna mwingine kama wewe, ee Mwenyezi-Mungu, na yote tunayoyasikia yanathibitisha kwamba hakuna Mungu mwingine ila wewe.
1 Mambo ya Nyakati 17:19-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, kwa ajili ya mtumishi wako, na kwa moyo wako mwenyewe, umeyatenda hayo makuu yote, ili yajulikane hayo matendo makuu yote. Ee BWANA, hakuna mwingine kama wewe, wala hakuna Mungu mwingine ila wewe, kwa kadiri tulivyosikia kwa masikio yetu.
1 Mambo ya Nyakati 17:19-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, kwa ajili ya mtumwa wako, na kwa moyo wako mwenyewe, umeyatenda hayo makuu yote, ili yajulikane hayo matendo makuu yote. Ee BWANA, hakuna mwingine kama wewe, wala hakuna Mungu mwingine ila wewe, kwa kadiri tulivyosikia kwa masikio yetu.
1 Mambo ya Nyakati 17:19-20 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee BWANA Mungu. Kwa ajili ya mtumishi wako, tena sawasawa na mapenzi yako, umefanya jambo hili kubwa sana na kujulisha ahadi hizi zote zilizo kubwa sana. “Hakuna aliye kama wewe, Ee BWANA Mungu, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe.