1 Mambo ya Nyakati 17:16-18
1 Mambo ya Nyakati 17:16-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha mfalme Daudi akaingia ndani ya hema na kuketi mbele ya Mwenyezi-Mungu, halafu akaomba, “Mimi ni nani, ee Mwenyezi-Mungu, na nyumba yangu ni nini hata unitukuze hivi? Isitoshe, umenifanyia mengine zaidi: Umenitolea ahadi juu ya vizazi vyangu vijavyo ee Mwenyezi-Mungu! Nikuambie nini zaidi, mimi Daudi mtumishi wako, kwa kunitukuza hivyo? Wewe unanijua mimi mtumishi wako.
1 Mambo ya Nyakati 17:16-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo akaingia Daudi mfalme, akaketi mbele za BWANA; akasema Mimi ni nani, Ee BWANA Mungu, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hadi hapa? Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Ee Mungu; hata umeleta habari ya nyumba yangu mimi, mtumishi wako, kwa miaka mingi inayokuja, nawe umeniangalia kama mtu mwenye cheo, Ee BWANA Mungu. Na Daudi akuambie nini tena zaidi kwa habari ya heshima aliyotendewa mtumishi wako? Kwa maana wewe umemjua mtumishi wako.
1 Mambo ya Nyakati 17:16-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo akaingia Daudi mfalme, akaketi mbele za BWANA; akasema Mimi ni nani, Ee BWANA Mungu, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hata hapa? Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Ee Mungu; hata umeleta habari ya nyumba yangu mimi, mtumwa wako, kwa miaka mingi inayokuja, nawe umeniangalia sawasawa na hali ya mtu mwenye cheo, Ee BWANA Mungu. Na Daudi akuambie nini tena zaidi kwa habari ya heshima aliyotendewa mtumwa wako? Kwa maana wewe umemjua mtumwa wako.
1 Mambo ya Nyakati 17:16-18 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za BWANA, akasema: “Mimi ni nani, Ee BWANA Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo? Kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Mungu, umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Umeniangalia kama mtu aliyetukuka kuliko watu wote, Ee BWANA Mungu. “Daudi aweza kukuambia nini zaidi kuhusu kumheshimu mtumishi wako? Kwa maana wewe unamjua mtumishi wako