Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 37:17-24

Ayubu 37:17-24 SRUV

Jinsi nguo zako zilivyo na moto, Hapo nchi ituliapo kwa sababu ya upepo wa kusini? Je! Waweza kuzitandaza mbingu pamoja naye, Ambazo zina nguvu kama kioo cha kuyeyushwa? Utufundishe ni maneno gani tutakayomwambia; Kwa kuwa hatuwezi kutoa hoja zetu maana tumo gizani. Je! Aambiwe kwamba nataka kunena? Au kuna mtu ambaye angetamani kumezwa? Na sasa watu hawawezi kuutazama mwanga ung'aao mbinguni; Lakini upepo ukipita huzitakasa. Kaskazini hutokea mng'ao wa dhahabu; Mungu huvikwa ukuu utishao. Yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea. Kwa hiyo watu humwogopa; Yeye hawaangalii walio na hekima mioyoni.

Soma Ayubu 37

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Ayubu 37:17-24

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha