Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenituma. Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli. Yuko mwingine anayenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli. Ninyi mlituma watu kwa Yohana, naye akaishuhudia kweli. Si kwamba ninaupokea ushuhuda wa wanadamu; lakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka.
Soma Yohana 5
Shirikisha
linganisha matoleo yote: Yohana 5:30-34
Hifadhi mistari, soma bila mtandao, tazama klipu za mafunzo, na zaidi!
YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video