Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 63

63
Faraja na Uhakikisho katika Bwana
Zaburi ya Daudi, alipokuwa katika Jangwa la Yudea.
1 # 1 Sam 23:14 Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea kiu,
Mwili wangu wakuonea shauku,
Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
2 # 1 Nya 16:11 Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,
Nizione nguvu zako na utukufu wako.
3 # Yn 3:16 Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai;
Midomo yangu itakusifu.
4Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;
Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
5 # Zab 17:15; Isa 25:6 Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono;
Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
6 # Zab 149:5 Ninapokukumbuka kitandani mwangu,
Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku.
7 # 2 Kor 1:10 Maana Wewe umekuwa msaada wangu,
Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
8 # Isa 26:9 Nafsi yangu inakuandama sana;
Mkono wako wa kuume unanitegemeza.
9Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiharibu,
Wataingia pande za nchi zilizo chini.
10Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga,
Watakuwa riziki za mbwa-mwitu.
11 # Sef 1:5 Bali mfalme atamfurahia Mungu,
Kila aapaye kwa Yeye atashangilia,
Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 63: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha