Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 34

34
Sifa kwa Kukombolewa katika Shida
Ya Daudi, alipojifanya mwenye kichaa mbele za Abimeleki, ndipo akafukuzwa na kumtoroka.
1 # 1 Sam 21:13-15 Nitamhimidi BWANA kila wakati,
Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
2 # Yer 9:24; 1 Kor 1:31 Katika BWANA nafsi yangu itajisifu,
Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.
3Mtukuzeni BWANA pamoja nami,
Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
4 # Zab 18:6; Yon 2:2; Mt 7:7; Lk 11:9 Nalimtafuta BWANA akanijibu,
Akaniponya na hofu zangu zote.
5Wakamwelekea macho wakatiwa nuru,
Wala nyuso zao hazitaona haya.
6 # Zab 3:4; 2 Sam 22:1 Maskini huyu aliita, BWANA akasikia,
Akamwokoa na taabu zake zote.
7 # Dan 6:22; Mwa 32:1; 2 Fal 6:17; Ebr 1:14 Malaika wa BWANA hufanya kituo,
Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
8 # 1 Pet 2:3 Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema;
Heri mtu yule anayemtumaini.
9 # Flp 4:19 Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake,
Yaani, wamchao hawahitaji kitu.
10Wana-simba hutindikiwa, huona njaa;
Bali wamtafutao BWANA hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema.
11Njoni, enyi wana, mnisikilize,
Nami nitawafundisha kumcha BWANA.
12 # 1 Pet 3:10-12 Ni nani mtu yule apendezwaye na uzima,
Apendaye siku nyingi apate kuona mema?
13 # 1 Pet 2:22 Uuzuie ulimi wako na mabaya,
Na midomo yako na kusema hila.
14Uache mabaya ukatende mema,
Utafute amani ukaifuatie.
15 # Ayu 36:7 Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki,
Na masikio yake hukielekea kilio chao.
16 # Law 17:10; Yer 44:11; Mit 10:7 Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya,
Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
17Walilia, naye BWANA akasikia,
Akawaponya na taabu zao zote.
18BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na waliopondeka roho huwaokoa.
19Mateso ya mwenye haki ni mengi,
Lakini BWANA humponya nayo yote.
20 # Yn 19:36 Huihifadhi mifupa yake yote,
Haukuvunjika hata mmoja.
21 # Zab 94:23 Uovu utamwua asiye haki,
Nao wamchukiao mwenye haki watahukumiwa.
22 # 2 Sam 4:9; Zab 103:4 BWANA huzikomboa nafsi za watumishi wake,
Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 34: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha