Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 147

147
Sifa kwa Mungu Kuutunza Yerusalemu
1Haleluya.
Msifuni Bwana;
Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu,
Maana kwapendeza, kusifu ni kuzuri.
2 # Kum 30:3; Isa 27:13; Yer 32:37; Eze 36:24 BWANA ndiye aijengaye Yerusalemu,
Huwakusanya waliotawanyika wa Israeli.
3 # Isa 61:1; Lk 4:18 Huwaponya waliopondeka moyo,
Na kuziganga jeraha zao.
4 # Mwa 15:5; Isa 40:26 Huihesabu idadi ya nyota,
Huzipa zote majina.
5 # 1 Nya 16:25; Nah 1:3 Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu,
Akili zake hazina mpaka.
6 # Zab 146:8 BWANA huwategemeza wenye upole,
Huwaangusha chini wenye jeuri.
7 # Efe 5:20 Mwimbieni BWANA kwa kushukuru,
Mwimbieni Mungu wetu kwa kinubi.
8 # Ayu 38:20 Huzifunika mbingu kwa mawingu,
Huitengenezea nchi mvua,
Na kuyameesha majani milimani.
9 # Ayu 38:41; Mt 6:26; Lk 12:24 Humpa mnyama chakula chake,
Wana-kunguru waliao.
10 # Hos 1:7 Hapendezwi na nguvu za farasi,
Wala hairidhii miguu ya mtu.
11BWANA huwaridhia wao wamchao,
Na kuzitarajia fadhili zake.
12Msifu BWANA, Ee Yerusalemu;
Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.
13Maana ameyakaza mapingo ya malango yako,
Amewabariki wanao ndani yako.
14Ndiye afanyaye amani mipakani mwako,
Akushibishaye kwa unono wa ngano.
15 # Ayu 37:12 Huipeleka amri yake juu ya nchi,
Neno lake lapiga mbio sana.
16Ndiye atoaye theluji kama sufu,
Huimwaga barafu yake kama majivu,
17Hutupa mvua ya mawe kama makombo,
Mbele ya baridi yake ni nani awezaye kusimama?
18Hulituma neno lake na kuviyeyusha,
Huuvumisha upepo wake, maji yakatiririka.
19 # Kum 33:4; Mal 4:4; Rum 3:2 Humhubiri Yakobo neno lake,
Na Israeli amri zake na hukumu zake.
20 # Kum 4:32; Mdo 14:16; Rum 3:1-2 Hakulitendea taifa lo lote mambo kama hayo,
Wala hukumu zake hawakuzijua.
Haleluya.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 147: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha