Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwa 8

8
Kupwa kwa Gharika
1 # Mwa 19:29; Kut 2:24; 1 Sam 1:19; Zab 105:42; 136:23; Kut 14:21; 15:10; Zab 104:7 Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua; 2#Mwa 7:11; 1 Fal 8:35; Ayu 38:37chemchemi za vilindi zikafungwa, pia na madirisha ya mbinguni, mvua kutoka mbinguni ikazuiliwa; 3#Mwa 7:24maji yakadumu kuondoka katika nchi; na mwisho wa siku mia na hamsini maji yakapunguka. 4Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina ikatua juu ya milima ya Ararati. 5Maji yakapunguka-punguka hata mwezi wa kumi; mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana. 6#Mwa 6:16Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya; 7#1 Fal 17:4akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi. 8Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi; 9#Kum 28:65bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani.
10Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili, 11#Lk 2:14njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi. 12Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe.
13Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka. 14Na mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, nchi ilikuwa kavu.
15Mungu akamwambia Nuhu, akisema, 16#Mwa 7:13; Zab 121:8Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe. 17#Mwa 1:22Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi. 18Basi Nuhu akatoka, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; 19kila mnyama, na kila kitambaacho, na kila ndege, kila kinachokwenda juu ya nchi kwa kabila zao, wakatoka katika safina.
Ahadi ya Mungu kwa Nuhu
20 # Law 11:1-31 Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. 21#Law 1:9; Kut 20:24; 2 Kor 2:15; Efe 5:2; Mwa 3:17; 6:17; Isa 54:9; Mwa 6:5; Zab 51:5; Ayu 14:4; 15:14; Yer 17:9; Rum 1:21; 3:23; Efe 2:1-3; Mwa 9:15BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. 22#Yer 33:20,25Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.

Iliyochaguliwa sasa

Mwa 8: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha