Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kut 6

6
Ukombozi wa Waisraeli Wahakikishwa
1 # Kut 11:1; 12:31 BWANA akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake.
2 # Mwa 17:1; 28:3; 35:11; Kut 3:13-15 Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; 3#Zab 68:4; Yn 8:58; Ufu 1:4nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao. 4#Mwa 15:18; 17:4,7,8Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya kukaa kwao hali ya ugeni. 5#Kut 2:24Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu. 6#Kut 3:17; 7:4; 15:13; Kum 26:8; 7:8; Zab 81:6; 136:11; 1 Nya 17:21; Neh 1:10Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa; 7#Kum 7:6; 29:13; 2 Sam 7:24; Mwa 17:7,8; Ufu 21:7; Zab 81:6nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri. 8#Mwa 15:18; 26:3Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA. 9Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu.
10BWANA akasema na Musa, akamwambia, 11Ingia ndani, ukaseme na Farao, mfalme wa Misri, ili awape ruhusa wana wa Israeli watoke nchi yake. 12#Yer 1:6Musa akanena mbele ya BWANA, akasema, Tazama, hao wana wa Israeli hawakunisikiza mimi; basi huyo Farao atanisikizaje, mimi niliye na midomo isiyo tohara? 13BWANA akanena na Musa na Haruni, akawaagiza wawaendee wana wa Israeli, na Farao, mfalme wa Misri, ili awatoe hao wana wa Israeli katika nchi ya Misri.
Nasaba ya Musa na Haruni
14 # Mwa 49:9; 1 Nya 5:3 Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba zao: wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; ni Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi; hao ni jamaa za Reubeni. 15#Mwa 46:10; 1 Nya 4:24Na wana wa Simeoni; ni Yemueli, na Yamini, na Ohadi, na Yakini, na Sohari, na Shauli mwana wa mwanamke wa Kikanaani; hao ni jamaa za Simeoni. 16#Hes 3:17-20; 26:57-58; 1 Nya 6:16-19; Mwa 46:11; 1 Nya 6:1Na haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, sawasawa na vizazi vyao; Gershoni, na Kohathi, na Merari; na miaka ya maisha yake Lawi ilikuwa ni miaka mia na thelathini na saba. 17Wana wa Gershoni; ni Libni, na Shimei, sawasawa na jamaa zao. 18#Hes 26:57; 1 Nya 6:18Na wana wa Kohathi; ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli; na miaka ya maisha ya huyo Kohathi ilikuwa ni miaka mia na thelathini na mitatu.
19Na wana wa Merari; ni Mali, na Mushi. Hizi ni jamaa za hao Walawi sawasawa na vizazi vyao. 20#Kut 2:1,2; Hes 26:59Huyo Amramu akamwoa Yokebedi ndugu ya baba yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia na thelathini na saba. 21#Hes 16:1; 1 Nya 6:37,38Na wana wa Ishari; ni Kora, na Nefegi, na Zikri. 22#Law 10:4; Hes 3:30Na wana wa Uzieli; ni Mishaeli, na Elisafani, na Sithri. 23#Rut 4:19,20; 1 Nya 2:10; Mt 1:4; Law 10:1; Hes 3:2Haruni akamwoa Elisheba, binti ya Aminadabu, umbu lake Nashoni; naye akamzalia Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. 24#Hes 26:11Na wana wa Kora; ni Asiri, na Elkana, na Abiasafu; hizo ni jamaa za hao Wakora. 25#Hes 25:7,11,12; Yos 24:33Na Eleazari mwana wa Haruni akamwoa mmoja miongoni mwa binti za Putieli; naye akamzalia Finehasi. Hawa ndio vichwa vya nyumba za mababa ya Walawi sawasawa na jamaa zao. 26#Kut 7:4; 12:17; Hes 33:1Hawa ni Haruni ye yule, na Musa ye yule, BWANA aliowaambia, akisema, Watoeni wana wa Israeli watoke nchi ya Misri sawasawa na majeshi yao. 27#Kut 32:7; 33:1; Zab 77:20Ni hao walionena na Farao mfalme wa Misri ili wawatoe wana wa Israeli watoke Misri; hao ni Musa ye yule, na Haruni ye yule.
Musa na Haruni Watii Amri za Mungu
28Ilikuwa siku hiyo BWANA aliponena na Musa katika nchi ya Misri, 29#Kut 7:2BWANA akamwambia Musa, akasema, Mimi ni BWANA; mwambie Farao mfalme wa Misri maneno yote nikuambiayo. 30#Kut 4:10; Yer 1:6Musa akanena mbele ya BWANA, Mimi ni mtu mwenye midomo isiyo tohara, Farao atanisikizaje?

Iliyochaguliwa sasa

Kut 6: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha