Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mhu 5

5
Uchaji, Unyenyekevu na Kuridhika
1 # Kut 3:5; Yos 5:15; Zab 89:7; Isa 1:12; 1 Sam 15:22; Zab 50:8; Mit 15:8; Hos 6:6 Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu;
Maana ni heri kukaribia ili usikie,
Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu;
Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.
2 # Zab 39:1; Mit 10:19; Mt 6:7 Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache. 3Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno. 4#Zab 66:13-14; Mwa 28:20; Hes 30:2; Zab 50:14; Isa 19:21; Yon 2:9Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.
5 # Mit 20:25; Mdo 5:4 Ni afadhali usiweke nadhiri,
Kuliko kuiweka usiiondoe.
6 # 1 Kor 11:10; 1 Tim 5:21 Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba umepitiliwa; kwani Mungu akukasirikie sauti yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako? 7#Kum 10:12; Mit 23:17; Mhu 12:13; Ebr 12:28Maana ndivyo ilivyo katika habari za wingi wa ndoto, na ubatili, na maneno mengi; walakini wewe umche Mungu.
8 # Mhu 3:16; Zab 12:5; Isa 57:15 Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu,
Aliye juu kuliko walio juu huangalia;
Tena wako walio juu kupita hao.
9Lakini, pamoja na hayo, manufaa ya nchi kwa kila njia ni mfalme anayejibidiisha kwa ajili ya shamba.
10Apendaye fedha hatashiba fedha,
Wala apendaye wingi hatashiba nyongeza.
Hayo pia ni ubatili. 11Mali yakiongezeka, hao walao nao waongezeka na mwenyewe hufaidiwa nini, ila kuyatazama kwa macho yake tu? 12Usingizi wake kibarua ni mtamu, kwamba amekula kidogo, au kwamba amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi.
13 # Mhu 6:1 Kuna na balaa mbaya sana niliyoiona chini ya jua, nayo ni hii, mali alizoziweka mwenyewe kwa kujinyima; 14na mali hizo zimepotea kwa bahati mbaya; naye akiwa amezaa mwana, hamna kitu mkononi mwake. 15#Ayu 1:21; Zab 49:17; 1 Tim 6:7Alivyotoka tumboni mwa mamaye, atakwenda tena tupu-tupu kama alivyokuja; asichume kitu cho chote kwa ajili ya kazi yake, hata akichukue mkononi mwake. 16#Mhu 1:3; Mit 11:29Hiyo ndiyo balaa mbaya sana, ya kwamba kama vile alivyokuja, vivyo hivyo atakwenda zake; naye amefaidiwa nini mwenye kujitaabisha kwa ajili ya upepo? 17#Zab 127:2Siku zake zote hula gizani, mwenye fadhaa nyingi, mwenye ugonjwa na uchungu.
18Tazama, mimi niliyoyaona kuwa ndiyo mema na ya kufaa, ni mtu kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote anayoifanya chini ya jua, siku zote za maisha yake alizopewa na Mungu; maana hilo ndilo fungu lake.
19Tena, kwa habari za kila mwanadamu, ambaye Mungu amempa mali na ukwasi, akamwezesha kula katika hizo, na kuipokea sehemu yake, na kuifurahia amali yake; hiyo ndiyo karama ya Mungu. 20#Kut 23:25Kwa kuwa mtu hatazikumbuka mno siku za maisha yake; kwa sababu Mungu humtakabali katika furaha ya moyo wake.

Iliyochaguliwa sasa

Mhu 5: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha