Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Sam 8

8
Waisraeli Waomba kuwa na Mfalme
1 # Kum 16:18; Amu 10:4; 12:14 Hata Samweli alipokuwa mzee, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli. 2Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba. 3#Mhu 2:19; Yer 22:15; Kut 18:21; Kum 16:19; 1 Tim 3:3; 6:10; Zab 15:5Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu.
4Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama; 5#Kum 17:14; 1 Sam 12:13; Hos 13:10; Mdo 13:21wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote. 6#Kut 32:31,32; 1 Sam 15:11; Mit 3:5Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba BWANA. 7#Kut 16:8; Mt 10:24,25; Lk 10:16; Yn 13:16; 1 Sam 10:19BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. 8Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe. 9Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.
10Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya BWANA. 11#Kum 17:16; 1 Sam 10:25; 14:52; 2 Nya 26:10-15Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake. 12Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake. 13Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji. 14#1 Fal 21:7Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake. 15Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake. 16Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng’ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe. 17Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake. 18#Ayu 27:9; Zab 18:41; Mit 1:25; Isa 1:15; Mik 3:4; Lk 13:25Nanyi mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyejichagulia; BWANA asiwajibu siku ile.
Waisraeli Wapewa Mfalme
19 # Isa 66:4; Yer 44:16 Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu; 20ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu. 21Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa BWANA. 22#Hos 13:11BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawafanyie mfalme. Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, Enendeni kila mtu mjini kwake.

Iliyochaguliwa sasa

1 Sam 8: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha