Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu; na hukumu zako ni za haki. Umetoa maamuzi yako, kwa haki na uthabiti. Upendo wangu kwako wanifanya niwake hasira, maana maadui zangu hawajali maneno yako. Ahadi yako ni hakika kabisa, nami mtumishi wako naipenda. Mimi ni mdogo na ninadharauliwa; hata hivyo sisahau kanuni zako. Uadilifu wako ni wa haki milele; sheria yako ni ya kweli. Taabu na huzuni vimenipata, lakini amri zako ndizo furaha yangu. Maamuzi yako ni ya haki daima; unijalie maarifa nipate kuishi.
Share
Read Zaburi 119
Save verses, read offline, watch teaching clips, and more!
YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy
Home
Bible
Plans
Videos