Zaburi 119:129-136
Zaburi 119:129-136 BHN
Maamuzi yako ni ya ajabu; kwa hiyo nayashika kwa moyo wote. Maelezo ya mafundisho yako huleta mwanga; huwapa akili watu wasiojua kitu. Nafungua kinywa kwa hamu kubwa, maana ninatamani sana amri zako. Unigeukie na kunionea huruma, kama uwatendeavyo wanaokupenda. Uniimarishie hatua zangu kama ulivyoahidi; usikubali mimi nitawaliwe na uovu. Unikomboe kutoka udhalimu wa binadamu, ili nipate kuzishika kanuni zako. Uniangazie uso wako kwa wema, unifundishe masharti yako. Macho yangu yabubujika machozi kama mto, kwa sababu watu hawaishiki sheria yako.