1
Waefeso 6:12
Biblia Habari Njema
Maana vita vyetu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu, wanaomiliki ulimwengu huu wa giza.
Compare
Explore Waefeso 6:12
2
Waefeso 6:18
Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu.
Explore Waefeso 6:18
3
Waefeso 6:11
Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.
Explore Waefeso 6:11
4
Waefeso 6:13
Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, mtakuwa bado imara.
Explore Waefeso 6:13
5
Waefeso 6:16-17
Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu. Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu.
Explore Waefeso 6:16-17
6
Waefeso 6:14-15
Basi, kaeni tayari. Ukweli na uwe kama mkanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani, na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu.
Explore Waefeso 6:14-15
7
Waefeso 6:10
Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu.
Explore Waefeso 6:10
8
Waefeso 6:2-3
“Waheshimu Baba na mama yako,” hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani, “Upate fanaka na kuishi miaka mingi duniani.”
Explore Waefeso 6:2-3
9
Waefeso 6:1
Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema.
Explore Waefeso 6:1
YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy
Home
Bible
Plans
Videos